JK kukamilisha uteuzi wa Bunge la Katiba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete, wiki ijayo atakamilisha uteuzi wa majina ya wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba, uteuzi unaoashiria kuanza kwa bunge hilo litakalokuwa na wajumbe 640.

Bunge hilo litakaloanza mwanzoni mwa mwezi ujao mjini Dodoma, litakuwa na kazi ya kuijadili na kuipitisha Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30 mwaka jana.

Wajumbe wengine watakaounda Bunge hilo ni 42 kutoka vyama vya siasa, 358 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na 81 kutoka Baraza la Wawakilishi.

Januari 2 mwaka huu, ilikuwa siku ya mwisho kwa Ikulu kupokea majina ya makundi mbalimbali ya kijamii ambayo yaliwasilisha mapendekezo ya majina ya watu ambao wangependa wawe wajumbe wa Bunge hilo. Makundi zaidi ya 50 yaliwasilisha majina yao.

Makundi hayo ni asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya Serikali, vyama vya kitaaluma, madhehebu ya dini na vyama vya siasa.

Kuanza kwa Bunge hilo kunatarajiwa kuwa na mvutano mkali kutokana na msimamo wa baadhi ya makundi hayo, hasa vyama vya siasa ambavyo vimekuwa vikipingana zaidi katika mfumo wa Serikali tatu uliopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, ilisema mbali na uteuzi huo, Rais Kikwete pia Ijumaa hii ataichapisha rasimu ya pili ya katiba katika Gazeti la Serikali.

Taarifa hiyo ilisema hata majina ya wajumbe wa Bunge la Katiba nayo yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013. Sheria hiyo inampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano kushauriana na Rais wa Zanzibar, kuteua wajumbe 201 wa Bunge la Katiba.

Pia inamtaka rais kuchapisha kwenye Gazeti la Serikali rasimu ya katiba ndani ya siku 30 baada ya kukabidhiwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

“Atateua wajumbe 201 wa Bunge la Katiba kutoka miongoni mwa majina yanayopendekezwa kwao na makundi yaliyotajwa ndani ya sheria hiyo,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Inaeleza kuwa rasimu ya katiba itachapishwa katika Gazeti la Serikali la Januari 24 mwaka huu.

Historia ya Tanzania kuwa na Katiba Mpya itakayotokana na maoni ya wananchi ilianza Desemba 31 mwaka 2011 wakati Rais Kikwete akilihutubia taifa

Alitamka wazi kuwa nchi sasa inahitajika Katiba Mpya ili kwenda na wakati. Baadaye aliwateua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba, tume ambayo ilianza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi Mei 3, mwaka 2012.

Tume hiyo ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kuandaa rasimu ya kwanza ya katiba ambayo ilitoka Juni 4 mwaka jana.

Baada ya kutolewa rasimu hiyo wananchi walipewa muda wa kuipitia na kuitolea maoni katika Mabaraza ya Katiba ya wilaya yaliyokaa kuanzia Julai 12 mpaka Septemba 2 mwaka jana.

CHANZO: MWANANCHI

Raza awang’akia wanaotaka atimuliwe uanachama CCM

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza (kulia)
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza (kulia)

 

Zanzibar. Mwakilishi wa Jimbo la Uzini (CCM), Mohamed Raza Dharamsi amesema hakuna kifungu wala mwongozo wowote wa CCM unaomzuia mwanachama kutotumia demokrasia ya kukosoa ikiwemo muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Raza alitoa msimamo katika majibu yake ya maandishi alipotakiwa kujieleza mbele ya kamati ya siasa ya jimbo na wilaya huko Uzini Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja hivi karibuni.

Alisema tuhuma namba moja hadi nane zilizotolewa zimejaa upotoshaji na chuki za mwandishi aliyetayarisha tuhuma hizo 16 kabla ya kujadiliwa na vikao vya siasa vya jimbo na wilaya.

“Hakuna kifungu wala mwongozo wowote wa chama unaozuia wanachama kukosoa na kutumia demorasia ya kutaka marekebisho ya katiba ya nchi yetu na sheria zake zinalinda haki ya kutoa maoni,” alisema Raza katika maandishi yake. Raza alisema kama kuna mtu katika chama anatafsiri ukosoaji ni kejeli au dharau ,hilo ni tatizo lake binafsi na wala si la chama au ukiukaji wa sheria za nchi.

Alisema kwamba kwa upande wake amesikitishwa sana kuwepo kwa watu wachache ndani ya CCM wanavyopenda kukitumia chama na vikao vyake halali kwa ajenda zao binafsi, badala ya  kutumia muda huo kukijenga chama na kinyume chake hutengeneza mifarakano.

“Mimi si mgeni hapa Zanzibar, nimeona na ninashiriki katika shughuli mbalimbali pia naona chama chetu kinavyojenga misingi ya kidemokrasia na uwazi wa hali ya juu,” alieleza Raza katika maelezo yake ya jumla ya barua yake.

Alisema ameshangazwa na hatua anazochukuliwa yeye wakati Katibu Mkuu wa CCM Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana katika ziara zake za kila siku amekuwa akikosoa utendaji wa viongozi wa chama na serikali licha ya kufanya kwake  hivyo wapo wasiofurahi ila anatimiza uwazi wa demokrasia ndani ya CCM.

Alisema kuwa wapo wanaotofautiana naye kimtazamo, jambo ambalo ni sahihi katika kufuata misingi ya demokrasia na kuonya si vyema kutumia vikao vya chama ili kuendeleza chuki dhidi yake kwa vile kitendo hicho kinaweza kubomoa badala ya kukijenga chama chao.

Raza anasisitiza kuwa mambo ambayo amekuwa akiyazungumza dhidi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar amekuwa akiyazungumza kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita akiwa hadharani na kwa maandishi na kwamba alichokifanya si kitu kipya.

“Mimi nimefanya kazi na vingunge wa siasa wa Muungano na Zanzibar, nimekuwa na kina Rais wa Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Hayati Mzee Rashid Kawawa,  Mzee John Malecela na  Hayati Dk  Omar Ali Juma, sasa nafanyakazi na Balozi Seif Ali Idd na Rais wa Zanzibar,Dk Ali Mohamed Shein,” alisisitiza Raza.

Alisema kwa bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa na kinyongo tokea aingie na kuwa Mwakilishi wa Jimbo la Uzini kutokana na kufanya mambo makubwa yaliowashinda wengine hasa katika sekta ya elimu, maji, huduma za jamii kwa kushirikiana na Serikali.

“Mkanda wa video unaochukuliwa kama ushahidi haieleweki kama uliangaliwa na kamati nzima au ulitazamwa na mtu mmoja kwa utashi wake,ameandika utitiri wa tuhuma na kudai zinanikabili bila ya kusadikika,” alieleza Raza.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabili Mwakilishi huo ni kuhoji uhalali wa Rais Jakaya Kikwete na Dk Ali Mohamed Shein kuunda Tume ya kukusanya maoni ya mabadiliko ya katiba na Bunge lake, kitendo ambacho kiinapoteza kodi za wananchi.

CHANZO: MWANANCHI

Mwanamke akamatwa na nyara za Serikali

 

index

WIZARA ya Maliasili na Utalii, imemkamata mwanamke mmoja, Mwajuma Hamisi akiwa na nyara za Serikali katika nyumba anayoishi kinyume cha sheria. Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam jana na wizara hiyo, ilisema Mwajuma alikamatwa Jumamosi saa 12:45 jioni katika eneo la Yombo Vituka na Askari wa Wanyamapori Kikosi cha Kupambana na Ujangili (KDU), Kanda ya Mashariki.

“Mwajuma alikutwa akiwa na nyara za Serikali ambazo ni ngozi mbili ndani ya nyumba anayoishi kinyume na sheria namba 5 ya kuhifadhi wanyamapori ya mwaka 2009,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, ilisema mtuhumiwa amekabidhiwa polisi kwa hatua zaidi za kisheria na amefunguliwa jalada namba CHA/RB/564/2014.

Askari hao, pia walimkamata raia wa China, Ling Tian Ijumaa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, akiwa na nyara mbalimbali.

Alisema Tian, alikutwa na hati ya kusafiri namba G28214172,

alikutwa akiwa na bangili 2 na mkufu mmoja wenye gololi 11 zilizotengenezwa kutokana na meno ya tembo.

Alisema mtuhumiwa amefikishwa polisi na kufunguliwa jalada namba JNIA/IR/16/2013, alikuwa akitokea Msumbiji kwenda China.

“Serikali haitalala hadi majangili wote wanapatikana na kufikishwa katika vyombo vya sheria, ilani inatolewa kuwa Tanzania si kichaka cha kupitishia meno ya tembo au magendo ya aina yoyote kama wanavyofanya watu sasa,” ilisema taarifa hiyo.

Alisema wizara inawahakikishia wananchi kuwa imejizatiti vilivyo kupambana na vitendo vya ujangili katika mapori yote, maeneo yote ya mipaka ya nchi yetu na kwenye viwanja vyote vya ndege pamoja na bandari zote.

Mabadiliko sasa kuhamia CCM, bungeni

Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Jenister Mhagama kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Emmanuel Herman
Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Jenister Mhagama kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi katika hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Emmanuel Herman

Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vitalazimika kufanya mabadiliko katika safu zake za uongozi kutokana na athari zilizosababishwa na mabadiliko yaliyofanywa na Rais Jakaya Kikwete katika Baraza la Mawaziri.

Juzi, Ikulu ilitangaza mabadiliko katika baraza hilo ambayo yaliwaweka kando mawaziri na manaibu waziri watano, huku sura kumi mpya zikiingia, mabadiliko ambayo yameacha nafasi mbili wazi katika sekretarieti ya CCM na nafasi nne katika uongozi wa Bunge.

Miongoni mwa walioteuliwa na kuapishwa jana ni waliokuwa wajumbe wa Sekretarieti ya CCM; Dk Asha-Rose Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Mwigulu Nchemba ambaye  ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Fedha.

Nchemba ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, wakati Dk Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alisema jana kuwa viongozi wa sekretarieti ya CCM wanapoteuliwa kushika nafasi nyingine za Serikali, wanalazimika kuziacha nyadhifa zao katika chama.

Nape alisema kwa maana hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete atalazimika kuteua watu wa kuziba nafasi za Dk Migiro na Nchemba. “Huu ni utaratibu tuliojiwekea katika chama kwamba viongozi wa sekretarieti hawatafanya kazi mbili za chama na Serikali, kwa hiyo viongozi hawa pia wataziacha nafasi za chama,” alisema Nape.

Hata hivyo Nape alisema utaratibu huo hauwagusi wenyeviti wa chama hicho wa mikoa, ambao wameteuliwa kuwa mawaziri ama manaibu waziri kwani uenyekiti si nafasi ya utendaji.

Katika uteuzi huo, Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Simiyu, Dk Titus Kamani aliteuliwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.

“Hawa wanaweza kuendelea na nyadhifa zao za uenyeviti katika chama, huku wakiwa na nyadhifa serikalini, hii haina athari kwa sababu siyo watendaji wakuu wa chama,” alisema Nape.

Bungeni

Bunge pia litalazimika kuchukua hatua za kuziba nafasi zilizoachwa wazi  na aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge pia Kiongozi wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Jenister Mhagama ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Wengine ni Mahmoud Mgimwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara na sasa ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala, Pindi Chana ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Naibu Spika, Job Ndugai alisema nafasi zilizoachwa wazi na wabunge hao zitazibwa kwa kuchagua wenyeviti wengine kwa mujibu wa Kanuni za Bunge.

“Mapema sana kamati za kudumu za Bunge zitakutana kabla ya Bunge la Katiba, nafasi ambazo zimeachwa wazi na walioteuliwa kuwa mawaziri zitazibwa kwa sababu kamati husika watachagua wenyeviti wao,” alisema Ndugai.

Kuhusu mawaziri walioachwa katika mabadiliko hayo, Ndugai alisema wao wanarejea kuwa wajumbe wa kamati.

“Kila mbunge ana haki ya kuwa kwenye kamati, kwa hiyo tutawapanga kwenye kamati mbalimbali na hawazuiwi kuchaguliwa kuwa wenyeviti ikiwa watapangwa kwenye kamati ambazo wenyeviti wao wamechaguliwa kuwa mawaziri,” alisema Ndugai.

Mawaziri walioachwa kwenye uteuzi huo ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck  Ole-Medeye,  Dk Terezya Huvisa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mazingira) na Benedict Ole-Nangoro,  aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Wengine ni Gregory Teu, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Philipo  Mulugo aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Viongozi hao wanaungana na wenzao wanne ambao uwaziri wao ulitenguliwa na Rais Kikwete mwishoni mwa mwaka jana kutokana na matokeo ya uchunguzi uliofanywa na Bunge kuhusu utekelezaji wa operesheni tokomeza ujangili.

Hao ni pamoja na waliokuwa Mawaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David, Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha.

CHANZO: MWANANCHI.

RAIS KIKWETE AFANYA MABADILIKO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa baadhi ya Mawaziri na kifo cha aliekuwa Waziri wa fedha na Uchumi Mh, Wiliam Mgimwa.

Mawaziri hao walijiuzulu kutokana na mapendekezo yaliyotolewa na wabunge kufuatia ripoti ya kamati mazingira iliyoundwa kuchunguza kadhia ya Operesheni tokomeza Ujangili iliyowasilishwa Bungeni katika kikao kilichopita.

Mawaziri walio jiuzulu katika kadhiya hiyo ni Sahamsi Vuai Nahodha aliekuwa  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Emmanuel Nchimbi aliekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki aliekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii na Dkt, Mathayo David Mathayo aliyekuwa Waziri wa aendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Katika mabadiliko ya Mawaziri na Manaibu Mawaziri Rais Kikwete amefanya amabadiliko kama ifuatavyo:-

1. OFISI YA RAIS


Hakuna mabadiliko.

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS


2.1 Waziri wa Nchi (Muungano) – Hakuna mabadiliko

Mhe. Eng. Dr. Binilith Satano MAHENGE (Mb)

Waziri wa Nchi (Mazingira).

Mhe. Ummy Ali MWALIMU (Mb)

Naibu Waziri

3. OFISI YA WAZIRI MKUU


Hakuna mabadiliko

4.0 WIZARA

4.1 WIZARA YA FEDHA

Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)

Waziri wa Fedha

Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)

Naibu Waziri wa Fedha (Sera)

Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)

Naibu Waziri wa Fedha

4.2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA


Hakuna mabadiliko

4.3 WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

4.3.1 Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria

Naibu Waziri – Hakuna mabadiliko

4.4 WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI


Hakuna mabadiliko

4.5 WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA

4.5.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.5.2 Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara

4.6 WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

4.7 WIZARA YA UJENZI


Hakuna mabadiliko

4.8 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

4.8.1 Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani

Naibu Waziri – Hakuna Mabadiliko

4.9 WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii

4.10 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

4.10.1 Waziri: Hakuna mabadiliko

4.10.2 Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi

4.11 WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

4.11.1 Waziri: Hakuna mabadiliko

4. 11.2 Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto

4.12 WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

4.12.1 Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Kaika Saning’o TELELE (Mb)

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi

4.13 WIZARA YA KAZI NA AJIRA


Hakuna mabadiliko

4.14 WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


Hakuna mabadiliko

4.15 WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

4.15.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.15.2 Mhe. George Boniface Taguluvala SIMBACHAWENE (Mb)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

4.16 WIZARA YA MAJI

4.16.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.16.2 Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji

4.17 WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

4.17.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.17.2 Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika

4.18 WIZARA YA UCHUKUZI

Hakuna mabadiliko

4.19 WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

4.19.1 Waziri – Hakuna mabadiliko

4.19.2 Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

4.20 WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

4.20.1 Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii

4.20.2 Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii

4.21 WIZARA YA NISHATI NA MADINI

Waziri – Hakuna mabadiliko


Naibu Waziri (Madini) – Hakuna mabadiliko


4.21.3 Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)

Naibu Waziri (Nishati)

NDOA YA OBAMA, MICHELLE SHAKANI

Rais Obama akiwa na mke wake Michelle Obama katika Pozi mbali mbali.
Rais Obama akiwa na mke wake Michelle Obama katika Pozi mbali mbali.

Marekani. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani vya Ikulu ya Marekani, wenza hao wamekuwa katika migogoro na Obama alilazimika kusherehekea sherehe za mwaka mpya mjini Hawaii akiwa na binti zake wawili, Sasha na Malia bila kuwepo Michelle.

Jarida la National Enquirer lilieleza kwamba katika moja ya matukio, Obama aliwahi kukutwa akiwa na mwanamke mwingine katika ‘mazingira ya kutatanisha’ wakati mkewe akiwa safarini.

Kutokana na ripoti iliyotolewa na Bombshel , Michelle na Obama wamekuwa wakilala vyumba tofauti ndani ya Ikulu. Michelle pia anajiandaa kuhama katika jumba lao pale Chicago ambalo wameishi wakati wa uchumba wao miaka 21 iliyopita na kwa msisitizo watajadili juu ya talaka.

Taarifa ilidai tatizo limeanza miaka minane iliyopita pale Obama alipodhamiria kujijenga kisasa. Ni mtoto wao Sasha ambaye aliumwa ugonjwa unaosababishwa na woga wa maisha unaoitwa Spinal Meningitis ndiyo uliowafanya waendelee kuwa pamoja.

Kitabu cha Anderson kinaelezea tatizo lilivyoanza baada ya Barack Obama kuamua kuingia kwenye siasa, ambapo Michelle alisikika akimwambia mumewe; “Wewe unajifikiria mwenyewe tu.”

Naye Barack Obama amesikika akisema: “Sikuwahi kufikiri kamwe kwamba ningelea familia mwenyewe siku moja.” Anderson anadai kuwa Obama amechoshwa na malalamishi ya mkewe.

“Nampenda sana Michelle lakini ananiumiza na ubishi wake wa kila mara,” alisikika akisema Obama na kuongeza kuwa; “Anaonekana ni mwingi wa machungu na hasira siku zote.”

Akizungumza na televisheni ya CBS ya Marekani, Anderson alidai kuwa ilikuwa nusura Michelle atembee nje ya ndoa kwa sababu ya upweke.

Kwa miaka mitano wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wao wa kupata watoto kabla Malia hajazaliwa. Walishajadili sana suala la kuasilia watoto (adoption) na marafiki zake wa karibu lakini kwa bahati nzuri Malia alizaliwa mwaka 1998 na kuondoa wazo hilo.


Jina kamili la Obama ni Barack “Barry” Hussein Obama, Jr, alizaliwa Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawaii, alikulia huko huko Hawaii na Indonesia, baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Jina kamili la mkewe ni Michelle LaVaughn Robinson, alizaliwa Januari 17, 1964 Chicago, Illinois.

Kukutana kwako

Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 katika mazingira ya kikazi, walifunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika Kanisa la Umoja wa Kristu la Trinity lililopo Chicago, Illinois.

Lakini vyanzo vingine vya taarifa zinadai kuwa ndoa haiko imara, hasa baada ya tukio la Obama kupiga picha za pamoja bila aibu na Waziri Mkuu wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt (46) wakati wa mazishi ya aliyekuwa rais wa kwanza wa Afrka Kusini, Neslon Madiba Mandela.

Obama akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, alikuwa akicheka na kumnong’oneza kitu waziri huyo mara kwa mara kwa muda wote, huku Michelle akiwa pembeni yake amenuna. Mara nyingi alikuwa akimshika shika mabega.

“Lakini kwa sasa Michelle anajiona kanyanyasika na kuaibishwa mbele ya dunia kwani picha hizo zilirushwa duniani kote kupitia televisheni, magazeti na mitandao mbalimbali. Alisikika akimtapikia Obama huku akisema “Nimechoshwa.”

Pia tatizo limekuzwa na safari ya kikazi ya Obama hivi karibuni kule Thailand ambayo ilimkutanisha na Waziri Mkuu mrembo kuliko pengine wote duniani , Yingluck Shinawatra.

Tarifa zaidi zilieleza kwamba usalama wa taifa nchini humo unafahamu kuhusu suala hilo, lakini umekuwa ukilichukulia kama suala binafsi na Michelle alionekana kukasirishwa kupita kiasi alipopata taarifa hizo.

“Baada ya tukio hilo Michelle aliamua kuwasiliana na mwanasheria wake akitaka kujua namna ya kuomba talaka na alimwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ilielezwa kwamba Michelle ataendelea kuishi mjini Washington DC hadi binti yao mdogo, Sasha (12) atakapomaliza elimu yake ya sekondari.

Binti yao mkubwa, Malia (15) tayari ameshaingia sekondari.
“Michelle (50) kwa sasa ataendelea kuishi kwenye Ikulu ya Washington hadi Obama atakapomaliza muda wake wa urais ili tu aweze kuonekana kama yupo, lakini aliweka wazi kabisa kwamba wataishi maisha tofauti,” ilieleza ripoti hiyo ikimkariri mmoja wa vyanzo kutoka Ikulu hiyo.

Ripoti hiyo ilikariri chanzo hicho kikieleza; “Michelle kwa sasa anaishi katika vyumba vya watumishi kwenye nyumba yao ya familia na anajiandaa kuchukua vifaa vyake na kuvipeleka kwenye nyumba yao binafsi ya Chicago”.

Taarifa nyingine ilieleza kwamba tayari mambo baina ya wanandoa hao yameshakuwa magumu kiasi kwamba wamekuwa wakiishi kwenye vyumba tofauti katika Ikulu ya Marekani.

Mgogoro wao

Barack na Michelle wamekuwa katika mgogoro kwa miaka kadhaa na wanalazimika kuwepo pamoja kwa sababu tu ya watoto wao na kulinda hadhi yake kisiasa. Lakini kwa sasa Michelle amekuwa mkali kweli kweli. Anaona kama amepuuzwa na kudhalilishwa mbele ya dunia nzima na amekuwa akipiga kelele akisema, “Nimevumilia vya kutosha”, taarifa zaidi zilieleza.

Kwa sasa Michelle anaonekana kupigania kukamilisha namna ya kupata talaka, lakini baadhi ya taarifa zinaeleza kwamba anafanya makusudi kuuchelewesha ili aweze kuukamilisha baada tu ya Obama kumalizia muda wake wa urais ambapo ataweza kupata Dola za Marekani 30 milioni kupitia mpango wa vitabu na zaidi ya dola 65 milioni kwa kuonekana hadharani.

“Kwa sasa Barack anaonekana kama amemwaibisha Michelle mbele ya dunia na kwa hili ni wazi kwamba atalilipa kwa gharama kubwa,” kilieleza chanzo kutoka Ikulu ya Marekani.

“Ni jambio lililo wazi kwa sasa kwamba Michelle ameshamwambia Obama kwamba anahitaji kuishi mbali naye, japokuwa kwa sasa imekuwa ni suala gumu kwa kuwa anahitaji aendelee kuonekana wakiwa pamoja kwa sababu muhimu, lakini wanapokuwa nyumbani wanaishi maisha tofauti ya kutengana,” kilieleza chanzo hicho.

Iwapo taarifa hizo ni sahihi, hii inamaanisha kwamba Michelle ameudhika kupindukia na hii si mara ya kwanza jambo hilo kutokea miongoni mwao.

Tangu Obama alipochaguliwa kuwa rais, vitabu viwili vimemtaja vikidai kwamba wenza hao walikaribia kutengana katika kipindi cha miaka yao ya mwanzo ya ndoa na hata Michelle alifikia hatua ya kutaka kuomba talaka akidai kwamba anaona maisha yake ya kisiasa yanawanyima furaha na kuwa pamoja nyumbani.

Mwaka 2009 mwandishi wa siku nyingi wa Washington, Richard Wolffe alisema kwamba ndoa hiyo ilikuwa sawa na iliyovunjika miaka tisa kabla kutokana na harakati za kisiasa za Obama zilizokuwa zikimsababisha asiwe karibu na familia kwa muda mrefu.

“Kulikuwa na mawasiliano kidogo sana na familia yake na hata mapenzi yalipungua. Michelle alikasirishwa sana na hali hiyo akilaumu kwamba mumewe anaonekana kuwa mbinafsi; ilimpa wakati mgumu sana,” aliandika Wollfe.

Wakati huo Michelle alilazimika kutulia kwa kuwa tayari alishakuwa mama, mbinti zao awili, Malia na Sasha kwa sasa wana miaka 15 na 12.

Mumewe ambaye walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa wakifanya kazi kwenye shirika moja la sheria mjini Chicago mwaka 1989, alikuwa ndiyo kwanza amechaguliwa kuwa Seneta wa Illinois na alikuwa akijipanga pia kuwania nafasi kwenye baraza la Congress.

Mke wa Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, Carla Bruni alipoulizwa katika moja ya vitabu kuhusu uzoefu wake wa maisha ndani ya Ikulu alijibu, ‘Acha kabisa! Usiulize ni kama jehanamu. Sikuwahi kuyafurahia’ ambapo Michelle alisema hakuwahi kuzungumza maneno ya aina hiyo.

Mwaka 2012 mmoja wa waandishi wa masuala ya siasa, Edward Klein alieleza kwamba Obama alionekana mwenye mawazo kupita kiasi, wakati ndoa yake ilipokuwa kwenye matatizo mwaka 2000 kiasi kwamba rafiki zake walihofu kwamba anaweza kujiua.

Alieleza kwamba Michelle alikuwa mwenye hasira kwa kuwa alimkataza Obama kuwania nafasi kwenye Congress, ushauri ambao hakuufuata na hata hivyo alishindwa kwenye uchaguzi.

“Baada ya kushindwa alirejea kwa Michelle kwa ajili ya kupata pumziko. Lakini Michelle hakuwa tayari kuonyesha huruma yoyote,” aliandika Klein aliyedai kwamba marafiki wa Michelle walimweleza kuwa tayari ameshafungua kesi akidai talaka.

CHANZO: MWANANCHI

Wapinzani wamgombea Zitto

 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mh. Zitto Kabwe.

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), ambaye ana mgogoro na chama chake, sasa anaonekana kugombewa na baadhi ya vyama vya siasa nchini. Hali hiyo imekuja baada ya baadhi ya wenyeviti wa vyama hivyo, kuzungumza na MTANZANIA Jumatatu na kumtaka kwa nyakati tofauti ajiunge na vyama vyao.

Katika mazungumzo yake, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alisema Zitto ana kila sababu ya kuhamia TLP ili aandaliwe kwa ajili ya kukiongoza chama hicho cha upinzani.

Kwa mujibu wa Mrema, Zitto akihamia TLP hatakuwa amepotea njia kwani chama hicho kina uzoefu wa siasa za upinzani.

“Zitto ni kifaa, ni jembe, ni mali inayouzika, ana soko na ni mti wenye matunda ndiyo sababu unapopolewa mawe kwa maana hana haja ya kujinadi.

“Akiamua kufanya uamuzi sahihi kwa kujiunga na TLP, hapa atakuwa amefika kwa sababu mimi nitakuwa wa mwisho kumnyanyasa Zitto.

“Tatizo kubwa linalomponza Zitto ni pale anapoamua kunyemelea uenyekiti wa watu, hilo ndilo kosa lake.

“Namwambia Zitto aje TLP na kama atakuja basi aje na watu wote wanaomuunga mkono huko Chadema.

“Kuna muda fulani niliacha biashara ya jumla nikaanza ya rejareja, ambayo nayo inalipa lakini Zitto akija, tutaanza kufikiria kufanya ile ya jumla maana anaiweza,” alisema Mrema.

Kwa upande mwingine, Mrema alisema Chadema wajifunze kutoka kwake kwani alipokuwa NCCR-Mageuzi, kuna wakati alitaka kuuawa kwa kisingizio kwamba alikuwa kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Dhambi ya usaliti ndiyo itaiua Chadema, kwa sababu baada ya kuona wanakubalika kwa wananchi, sasa wakataka kuvidhoofisha vyama vyote vya upinzani ili wabaki wao tu na sasa wanaona matokeo yake,” alisema Mrema.

Naye, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, alisema Zitto ana vigezo vyote vya kuwa mwanachama wa chama hicho, kwa kuwa anakubalika kwa wananchi.

“Sura ya tatu, ibara ya tisa ya Katiba yetu inaeleza masharti ya kujiunga na chama ambayo ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania, mhusika kuwa na umri wa miaka 18 na pia awe na akili timamu.

“Zitto ni Mtanzania na sifa zote hizo anazo, kwa hiyo, kama atatekeleza hayo basi anunue kadi ya chama chetu na tunamkaribisha NCCR.

“Lakini kuhusu kinachoendelea huko Chadema, kwa bahati mbaya siwezi kukizungumzia kwa sababu mimi siyo msemaji wao,” alisema Mbatia.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kwa kifupi kwamba kinachoendelea Chadema ni kukua kwa demokrasia.

“Hilo siyo jambo jipya, ni jambo la kawaida katika vyama vikubwa kama Chadema, kwa hiyo watu wasishangae, waone hali hiyo kama ya kawaida kisiasa,” alisema Profesa Lipumba.

Wakati hao wakisema hayo, Peter Mziray ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha PPT-Maendeleo, alisema Zitto anatakiwa kuondoka Chadema kwa kuwa hakubaliki tena.

Kutokana na hali ilivyo, alisema Zitto hatakiwi kung’ang’ania demokrasia ndani ya chama hicho, kwani atawafanya watu waanze kujiuliza anataka nini katika chama hicho.

“Kwa jinsi ninavyoona, makosa yake hayasameheki, ni kama anaonekana amepindua nchi ambapo adhabu yake ni kifungo. Zitto hajapindua nchi bali anaonekana anataka kupindua chama na adhabu yake ni kufukuzwa.

“Ni vigumu, Zitto kuachwa salama kwa sababu yanayomhusu ndani ya chama chake ni mengi na yale aliyoyapeleka mahakamani na kushinda ni zuio tu siyo kesi ya msingi.

“Pamoja na hayo, taarifa nilizonazo ni kwamba, ule muhtasari wa kikao kilichomfukuza ambao aliuomba, anaweza akapatiwa ili akate rufani kwa sababu ni haki yake ya msingi ya kikatiba, lakini anaweza asishinde.

“Katika suala la kujiunga katika chama chetu, akitaka kuja suala la kumkubalia au kumkatalia ni suala la mazungumzo, kwa sababu yeye ni mwanasiasa kijana, anahitaji kujifunza.

“Pia anahitaji kubadilika na Chadema inahitaji kubadilika kwa sababu haya mambo yao yanatuchelewesha wanamageuzi. Hivi mambo kama ni haya, nchi tutaishika lini kwa mtindo huu,” alihoji Mziray.

CHANZO: MTANZANIA

MATUKOIO YALIOVUTA HISIA ZA WATU WENGI 2013

Leo tarehe 01/01/2014 tumeanza kuhesabu tarehe ya mwaka mpya wa 2014 ikiwa tayari tumeshauwaga mwaka wa 2013. Ni matumaini yangu wengi wetu ni wenye furaha kwa kubarikiwa neema hii ya kuushuhudia mwaka mpya katika hali ya amani hapa nchini petu, kwa hili hatuna budi kujipongeza.

Licha ya kuuanza mwaka mpya lakini mwaka uliyopita utabakia kuwa kumbukumbu kwetu na vizazi vijavyo kutokana na matukio yaliyojitokeza hapa nchini.

Yametokea mengi ambayo yameipa sifa kubwa nchi yetu lakini mengine ni matukio ya aibu na ya kufedhehesha hasa kwa nchi zinazo endeshwa katika misingi ya utawala bora kama hapa kwetu.

Katika mwaka ulioisha tumeshuhudia uendelezwaji mzuri wa mchakato wa upatikanaji wa Kaitba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo tayari rasimu ya pili ya katiba imeshazinduliwa ikisubiri kujadiliwa katika bunge maalum la Katiba litakaloanza mwezi ujao baada ya maboresho ya ile rasimu ya awali.

Ni matumaini yetu kwa wale watakao bahatika kuingia katika Bunge hili watatuletea Katiba yenye kujali maslahi ya Taifa na Wananchi badala ya maslahi ya makundi yao wanayo yawakilisha.

Nchi yetu ya Tanzania katika kipindi cha mwaka 2013 ilikumbwa na matukio mengi kama nilivyo eleza hapo awali ambayo mengine yameipa sifa kubwa lakini pia mengine ni ya kutia aibu mbele ya Mataifa mengine.

Kutokana na matukio yaliyojitokeza nitajaribu kuorodhesha baadhi ya matokeo yaliyotokea mwaka uliopita ambayo naamini yatakuwa ni kumbukumbu kwa mwaka huu na miaka mengine inayofuata.

MASHAMBULIZI.

Kama ilivyokuwa mwaka 2012 kuibuka kwa mashambulizi ya watu wa taasisi Fulani na mwaka wa 2013 mashambulizi bado yamekuwa yakiendelea.

Katika mwaka wa 2013 tumeshuhudia kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Nd. Absalom Kibanda na watu wasiojulika nyumbani kwake akiwa anarejea kazini.

Pia tumeshuhudia kushambuliwa kwa mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi ambae amefariki akiwa matibabuni nchini Afrika kusini kwa kushambuliwa na watu wanosadikiwa kuwa ni majambazi nyumbani kwake.

Licha ya mashambulizi haya bado hakuna taarifa yoyote ya kufikishwa katika vyombo vya sheria wahalifu waliotenda unyama huu na hakuna taarifa yoyote iliyotolewa yenye kuridhisha.

MIRIPUKO YA MABOMU

Mei 5 mwaka 2013 tumeshudia tukiop la kusikitisha la kuripuliwa kwa bomu kwa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph, mfanya kazi wa Olasiti jijinin Arusha  ambapo watu watatu walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.

Mwezi mmoja tu baada ya shambulizi la Arusha tunmeshuhudia tena shambulizi la bomu katika mkutano wa kufungakampeni za Chadema katika uchauguzi mdogo wa madiwani Mkoa wa Arusha ambapo pia watu watatu walifariki dunia na wengine kujeruhiwa.

Mashambulizi haya yamekuwa yakijenga picha mbaya kwa Taifa letu hasa kutoka na na sifa ya kuwa Nchi yetu ni kisiwa cha amani.

MASHAMBULIZI YA TINDIKALI.

Katika kipindi cha mwaka 2013 vitendo vya umwgiwaji watu Tindikali vimeongezeka kwa kiwango kikubwa chini kutokana na watu mbalimbali kukutwa mashambulizi haya.

Vitendo hivi vimeripotiwa kwa wingi zaidi Zanzibar kwani tumeshuhudia matukio tofauti ya umwagiwaji wa tindikali kwa baadhi ya watu na hata viongozi wa dini.

Tumeshuhudia kumwagiwa tindikali kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo Bwana Mohd Omar Said (Kidevu) akiwa nyumbani kwake. Pia Padri wa kanisa Katoliki Parokia ya Cheju Anselmo Mwang’ambwa anae alimwagiwa tindikali akiwa anatoka duakani maeneo ya Mlandege Zanzibar.

pia wasichana wawili Kate Gee na Kirstie Trup raia wa Uingereza  nao walimwagiwa Tindikali maeneo ya Mji Mkongwe wakati wakiwa katika matembezi ya jioni, ambapo tukio hili

Siku chache baada ya tukio hilo jina la Tanzania lilichafuka katika ramani ya kimataifa kutoka na vyombo mbalimbali vya habari kulizungumza suala hili kwa hisia kali mbele ya jamii ya Kimataifa.

HALI MBAYA YA BUNGE.

Katika kipindi cha mwaka 2013 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekuwa katika hili imbaya inayotia aibu kwa taifa kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu vilivyokuwa vikifanywa na wabunge.

Ndani ya bunge kumekuwa na kauli zisizo stahili kutolewa na watu wenye dhamana ya kuwawakilisha wananchi katika chombo kikubwa cha nchi kama bunge.

Pia kumeibuka vitendo vya vurugu mara kadhaa ndani ya Bunge jambo linalo lijengea taswira baya bunge letu.

ZIARA ZA MARAIS WA CHINA NA MAREKANI.

Ujio wa Rais wa Marekani Barack Obama

Nisiku mbili zakihistori kuwahi kutokea Tanzania kwa kwani tumeshuhudia maandalizi ya aina yake kabla ya kuwasili Julai 1 mwaka jana na kuondoka Julai 3.

Katika ziara hii tumeshuhudia barabara kadhaa zikifuungwa ili kutoa nafasi kwa ugeni aliokuja nao akiambatana na familia yake pamoja na makachero kadhaa wa usalama kutoka Marekani.

Pia tulishuhudia wafanya biashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga wkifkuzwa katika maeneo yao ya biashara ili kuweka maandhari mazuri katika kipindi chote cha ziara yake, hasa maeneo ya Posta, Kariokoo Manzese na maeneo mengine ambapo msafara wake ulipita.

MAUAJI YA KUTUMIA SILAHA

Mwaka huu pia kulikithiri kwa mauaji ya  kinyama kwa kutumia silaha ambapo watu kadhaa walijikuta wakipoteza maisha na wengine kujeruhiwa, kutokana na vitendo hivyo vilivyoonekana kushika kasi nchini

Miongoni mwa matukio hayo ni kuuwawa kwa risasi mnamo Februari 7 Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mianara miwili akiwa anelekea kuongoza ibada ya Jumapili katika Kanisa la mtakatifu Theresia lililopo Beit el Rass mjini Zanzibar.

Mauaji mengine yalitokea Agosti 7 kwa mfanyabiashara maarufu wa madini Erasto Msuya kuuawa kwa kupigwa risasi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro. Msuya alikuwa anamiliki vitegauchumi kadhaa na kuaminika kama mfanyabiashara aliyekuwa akiongoza kwa utajiri Mirerani aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20

MGOGORO WA GESI MTWARA

Maelfu ya wakazi wa Mkoa wa Mtwara waliandamana wakipinga uamuzi wa Serikali kusafirisha gesi kwa njia ya bomba, kutoka mkoani hapo kwenda Dar es Salaam kwa lengo la kutaka rasilimali hiyo ibaki Mtwara.

Kufuatia fujo na vurugu zilizotokea katika maandamano hayo risasi na mabomu yalirindima, hali iliyozua hofu na tafrani mkoani hapo.

SAKATA LA SHEIKH PONDA

Tukio la kujeruhiwa kwa Katibu wa Jumuiya ya Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa Ponda ilikuwa miongoni mwa habari zilizoibua mjadala mzito huku kukiwepo na hali ya sintofahamu kama kiongozi alijeruhiwa kwa risasi au kitu chenye ncha kali.

Mkasa huo wa aina yake ulitokea Agosti 10, mwaka huu majira ya saa 12: 15 za jioni eneo la Barabara ya Tumbaku karibu na Fire, mkoani Morogoro mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Kiislamu lililofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja Cha Ndege, Kata ya Saba Saba.

Baada ya tukio hilo, uvumi ulisambaa maeneo mbalimbali nchini ukidai kuwa Shekhe Ponda amepigwa risasi na polisi na kufariki dunia.

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Tatizo la madawa ya kulevya limeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha mwaka 2013 ambapo kumekuwa kukiripotiwa matukio ya kukamatwa wasafirishaji wa madawa hayo hapa nchini na nje ya nchi.

KUPOROMOKA KWA GHOROFA

Ilikuwa ni asubuhi ya Machi 29 ambapo jengo la ghorofa 16 lililokuwa linajengwa katika Mtaa wa Indira Gandhi  jijini  Dar es Salaam, liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 36 na wengine kadhaa kufunikwa na kifusi.

Kuporomoka kwa ghorofa hilo kulizua huzuni, taharuki na simanzi kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye eneo la tukio kutaka kufahamu nini kimetokea hali iliyosababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali katikati ya jiji.

OPERESHENI TOKOMEZA

Operesheni  hii iliyolenga kupambana na vitendo vya ujangili dhidi ya wanyamapori ilianza rasmi Oktoba 5, mwaka huu katika hifadhi za taifa, mapori ya akiba na mbuga za wanyama huku ikishirikisha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Polisi, Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Idara ya Wanyamapori.

katika operesheni hii kuna matendo mengi ya uvunjifu wa hki za binadamu vilivyofanywa na Vikosi vilivyokuwa vikiendesha opersheni hii vikiwemo vitendo vya ubakaji, kupiga watu ovyo pamoja na mauaji ya raia wasio na hatia.

Kutokana na matendo hayo kulipelekea baadhi ya Mawaziri kuwajibika kisiasa kama ilivyopendekezwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwsilishwa kwa ripoti ya tume ya ardhi, maliasili na mazingira kufichua vitendo hivyo.

Mawaziri walio wajibika ni aliekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Dkt, Emmanuel Nchimbi, aliekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh, Shamsi Vuai NAhodha, aliekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na aliekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mathayo David Mathayo.

Baraza la Mawaziri sasa laiva

Mawaziri, wabunge waitwa Dar
*Dk. Nchimbi, Kagasheki wamo
*Baadhi waanza kusherehekea

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kuipanga upya safu ya Baraza lake la Mawaziri wakati wowote, huku baadhi ya wabunge na mawaziri wakitakiwa kusitisha mapumziko yao ya mwisho wa mwaka na kurejea jijini Dar es Salaam haraka.

Miongoni mwa wabunge waliositisha mapumziko yao na kurejea nchini ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi, aliyekuwa nchini Afrika Kusini na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, aliyekuwa Uswisi.

Wabunge hao walipoteza nafasi zao za uwaziri baada ya ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuwagusa mawaziri hao kwamba walishindwa kuwajibika katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili.

Dk. Nchimbi anapewa nafasi ya kurejea kwenye Baraza la Mawaziri kutokana na kushiriki kwake kuipinga operesheni hiyo, ambayo kwa kiwango kikubwa ilikuwa chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, na kwamba alishawahi kumuandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akiipinga.

Kwa upande wake Kagasheki, anatajwa kurudi kwenye Baraza la Mawaziri kutokana na kubainika kwamba hakuwa na kosa na kwamba operesheni hiyo ilitekelezwa zaidi kijeshi na haikuwa chini ya wizara yake moja kwa moja.

Aidha Kagasheki anatajwa kuwa mmoja wa waliokuwa mawaziri hodari kutokana na uwezo wake wa kufuatilia mambo, ambapo akiwa ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii, alianza harakati za kukomesha biashara haramu ya pembe za ndovu.

Wakati Kagasheki na Dk. Nchimbi wakipewa nafasi ya kurejea kwenye Baraza la Mawaziri, pia zipo taarifa kwamba wapo baadhi ya wabunge wataingia kwa mara ya kwanza kwenye baraza hilo, huku wengine wakirudishwa kwa mara ya pili.

Taarifa za uhakika kutoka kwa watu wa karibu wa baadhi ya wabunge, zimebainisha kwamba jana Rais Kikwete aliwaita Ikulu wabunge wawili vijana, hata hivyo haikujulikana waliitwa kwa sababu gani.

Baadhi ya wabunge wanaotajwa kujumuishwa kwa mara ya kwanza kwenye baraza hilo ni Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, sambamba na mmoja wa wabunge vijana kutoka mikoa ya Iringa na Njombe.

Wakati wabunge hao wakiitwa Ikulu, zipo taarifa za uhakika kwamba mawaziri wote wametakiwa kusitisha mapumziko yao ya mwisho wa mwaka na kurejea Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya kutajwa kwa baadhi ya wabunge kuingia kwenye Baraza la Mawaziri imewatia hofu baadhi ya mawaziri, hasa wale walionyooshewa vidole na chama chao kwamba ni mawaziri mizigo.

Mawaziri waliotajwa na CCM kuwa ni mizigo wamekuwa hawana matumaini ya kurejea kwenye baraza hilo na kwamba wanaamini wao ndio watakuwa wa kwanza kutemwa.

Wakati baadhi ya mawaziri wakiwa na hofu, zipo taarifa kwamba mmoja wa wabunge wanaotoka Mkoa wa Mbeya ameshaanza kufanya sherehe, akiamini kwamba amejumuishwa kwenye Baraza la Mawaziri.

Aidha imebainika kwamba wapo baadhi ya manaibu waziri wameshaanza kujipigia debe ili kupandishwa na kuwa mawaziri kamili.

Mchakato huo wa kujipigia debe unachagizwa na utaratibu wa Rais Kikwete wa kuwapandisha hadhi manaibu waziri kuwa mawaziri kamili.

Tayari baadhi ya Manaibu Waziri kama Amos Makala, Lazaro Nyalandu na January Makamba,  Aggrey Mwanri na Angela Kairuki, wameshaanza kutajwa kuwa wanastahili kuwa mawaziri kamili.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, anatajwa kuwa miongoni mwa Manaibu Waziri wanaoweza kusalia kwenye Baraza la Mawaziri, kutokana na utendaji wake, lakini hawezi kupandishwa hadhi kutokana na makosa madogo aliyowahi kuyafanya, kama vile kushindwa kutofautisha nchi ya Zambia na kisiwa cha Zanzibar, hali iliyoonesha kuishushia hadhi Serikali ya Rais Kikwete, kwa kuwa na kiongozi asiyejua historia na jiografia ya nchi yake.

Utamaduni wa kupandisha manaibu waziri

Dhana ya manaibu waziri hao kupandishwa inatokana na hatua ya Rais Kikwete kuwahi kuwapandisha Dk. Nchimbi, aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Aidha Ezekiel Maige kabla ya kupandishwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alikuwa naibu waziri wa wizara hiyo, wakati huo ikiwa chini ya Shamsa Mwangunga.

Balozi Kagasheki kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alikuwa naibu waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mara baada ya Rais Kikwete kuingia madarakani, mwaka 2006 alimpandisha aliyekuwa Naibu Waziri wa Maji na Mifugo wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Anthony Diallo, kuwa Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo.

William Ngeleja, aliyekuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, alipandishwa hadhi na kuwa waziri kamili wa wizara hiyo, kabla ya kutemwa kwenye mabadiliko ya mawaziri yaliyofanyika Mei, mwaka 2013.

Aidha Waziri wa sasa wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, awali alikuwa Naibu Waziri wa Ujenzi.

Dk. Cyril Chami, ambaye ameanza kupigiwa chapuo la kurejea kwenye baraza jipya, kabla ya kupandishwa hadi kuwa Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara na kutemwa mwaka 2012, alianzia kwenye unaibu waziri kwenye wizara hiyo.

Mawaziri wengine ambao walianzia kwenye nafasi ya unaibu waziri ni Celina Kombani, ambaye kabla ya kuwa waziri kamili wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), alikuwa Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Kwa upande wake, aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo, Dk Mathayo, kabla ya kupewa nafasi hiyo alianzia kwenye nafasi ya Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika.

Historia hiyo ya Rais kuwapa hadhi manaibu waziri kuwa mawaziri inatoa nafasi kwa manaibu wengi kuamini kuwa huenda wakapandishwa, hata hivyo hali ni tofauti kwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, ambaye amekosa bahati ya kupandishwa kuwa waziri kamili, ingawa ni mmoja wa manaibu waziri wa muda mrefu waliozunguka kwenye wizara mbalimbali.

Dk. Migiro na uwaziri
Kwa upande wake, Dk. Asha-Rose Migiro anapewa nafasi kubwa ya kuwemo kwenye Baraza la Mawaziri, kutokana na historia ya Rais Kikwete ya kutoa nafasi ya uwaziri kwa watu anaowateua kuwa wabunge, ambapo kwenye idadi ya wateule wake nane, tayari watano amewapa nafasi ya uwaziri.

Wabunge hao ni Shamsi Vuai Nahodha, aliyekuwa akiongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Profesa Makame Mbarawa, anayeshikilia Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Wateule wengine wa Rais kwenye ubunge ambao wameteuliwa kuwa mawaziri ni Profesa Sospeter Muhongo, anayeshikilia Wizara ya Nishati na Madini, Saada Mkuya na Janet Mbene, ambao ni manaibu waziri wa Wizara ya Fedha.

Wakati Dk. Migiro na wabunge wengine wakipewa nafasi ya kuwemo kwenye Baraza la Mawaziri, joto linabaki kwenye nani atakwenda wizara gani.

Wizara zinazoonekana kuwa ni mtihani kwa Rais Kikwete kumpa mtu sahihi ni Wizara ya Fedha, ambayo inashikiliwa na Dk. William Mgimwa, ambaye kwa sasa ni mgonjwa.

Hata hivyo, Dk. Abdallah Kigoda, anayeshikilia Wizara ya Viwanda na Biashara kwa sasa, anatajwa kuweza kuimudu wizara hiyo, huku Zakia Meghji akitajwa kuwa na nafasi kubwa ya kurudi kwenye Baraza la Mawaziri, ili kuiongoza Wizara ya Maliasili na Utalii.

Dk. Migoro anapewa nafasi ya kurejea kwenye wizara yake ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, huku Bernad Membe, anayeshikilia wizara hiyo, akipewa nafasi ya kurudishwa Wizara ya Mambo ya Ndani, aliyoihudumia kwa kipindi kifupi akiwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Uteuzi wa nafasi ya uwaziri kimikoa
Kama Rais Kikwete ataendeleza utaratibu wake wa kuchagua mawaziri kulingana na mikoa yao na kuamua kutomrejesha Nchimbi kwenye Baraza la Mawaziri, anaweza kuteua mmoja kati ya wabunge hawa, Mbunge wa Viti Maalumu, Mhandisi Stella Manyanya, Jenister Mhagama (Peramiho), Vita Kawawa (Namtumbo) au Mhandisi Ramo Makani (Tunduru Kaskazini) ili kujaza nafasi ya Nchimbi.

Endapo Kagasheki hatarejea, ni wazi turufu ya kuwemo kwenye Baraza la Mawaziri inaweza kumuangukia Jason Rweikiza (Bukoba Vijijini), Charles Mwijage (Muleba Kaskazini), Deogratius Ntukamazina (Ngara) au Asumpta Mshama (Nkenge).

Nafasi ya Dk. David Mathayo, huenda ikawa kaa la moto kwa Rais Kikwete kufanya maamuzi ya kumpata mtu sahihi, kwani idadi ya wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro ni ndogo na kwamba wengi wao wameshashikilia wizara, ukimuondoa Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, ambaye wachambuzi wa masuala ya siasa hawampi nafasi sana ya kuingia kwenye Baraza la Mawaziri.

Kauli ya Ikulu
MTANZANIA Jumatano lilimtafuta Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, Premi Kibanga, ili kujua ukweli wa habari hizo, lakini alisema hajui chochote.

“Mimi niko Tanga, sijui kinachoendelea,” alisema Kibanga kwa kifupi, alipozungumza kwa simu na gazeti hili.

Operesheni Tokomeza inarudi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amesema Operesheni Tokomeza Ujangili iliyositishwa kwa muda kutokana na utekelezaji wake kukumbwa na kasoro na kusababisha mawaziri wake wanne kuwajibika kisiasa, itaendelea baada ya kukamilika kwa matayarisho ya awamu yake ya pili.

Akizungumza katika salamu zake za Mwaka Mpya jana, Rais Kikwete alisema: “Tunakamilisha matayarisho ya kuanza awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza. Ni muhimu kuendelea nayo kwani tusipofanya hivyo majangili wataendelea na vitendo vyao viovu.

“Wakati nikilihutubia Bunge Novemba 7, mwaka jana niliagiza ifanyike sensa katika Pori la Hifadhi la Selous. Hali ni mbaya, sensa imekamilika lakini taarifa yake inatisha. Kuna tembo 13,084 tu wakati mwaka 1976 walikuwa na tembo 109,419.”

Rais Kikwete ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku 12 tangu Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ilipotoa ripoti yake iliyoeleza athari mbalimbali za operesheni hiyo, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji, uharibifu wa mali na mauaji ya binadamu na mifugo.

Ripoti hiyo ilisababisha, Rais kutengua uwaziri wa Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi), Dk David Mathayo (Mifugo na Uvuvi) na Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), baada ya wizara zao kutajwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa operesheni hiyo.

Hata hivyo, Rais alisema mtindo wa mzigo wa makosa ya watumishi wa umma kubebwa na viongozi wa kisiasa pekee, tena wasiokuwa na hatia ya moja kwa moja, siyo sahihi. “Lazima kila mtu abebe mzigo wake inavyostahili. Ni matumaini yangu pia kwamba katika siku za usoni kunapotokea matatizo ya namna hii uchunguzi uwe wa kina ili wale hasa waliohusika na kutenda makosa wawajibishwe.

“Uwajibikaji wa wana-siasa peke yao hautoshi, kwani huwaacha waharibifu waendelee na kazi isivyostahili. Mtindo huu utawafanya watumishi wasione umuhimu wa kutokurudia makosa. Hata hivyo, pale kwenye ushahidi wa wazi kwamba kiongozi wa kisiasa angeweza kuchukua hatua za kuzuia madhara lakini hakufanya hivyo lazima kiongozi huyo awajibike.”

Kuhusu umuhimu wa kuendelea na operesheni hiyo alisema: “Tusipoendelea na operesheni hii, baada ya miaka michache ijayo hakutakuwa na tembo hata mmoja. Zoezi la kuondoa mifugo katika mapori ya hifadhi ya taifa litaendelea na katika awamu ya pili ya operesheni hii, washiriki watasisitizwa kutokutenda maovu yaliyofanyika katika awamu ya kwanza.”

Alisema tangu mwaka 2010 Serikali ilianzisha operesheni mbalimbali kupambana na ujangili wa wanyamapori na uvunaji haramu wa rasilimali za misitu, lakini kutokana na majangili kutumia silaha na mbinu, aliamua kuhusisha vyombo vingine vya ulinzi na usalama na hapo ndipo ilipoanza Operesheni Tokomeza.

“Pamoja na matatizo yake, katika Operesheni Tokomeza tumebaini mitandao ya ujangili na wahusika kadhaa wametiwa nguvuni. Mitandao hiyo inahusisha watu wa aina mbalimbali, wamo raia wa kawaida, watu maarufu, watumishi wa idara mbalimbali za Serikali wakiwamo wa Idara za Wanyamapori na Misitu,” alisema.

Alisema katika operesheni hiyo watu 1,030 walikamatwa pamoja na silaha za kijeshi 18, za kiraia 1,579 na shehena kubwa za meno ya tembo na nyara mbalimbali.

“Niliagiza operesheni hii isitishwe na uchunguzi ufanyike kubaini kasoro zake sambamba na waliofanya makosa wachukuliwe hatua. Wakati suala hilo likiendelea, Bunge likaunda kamati na matokeo yake mliyaona, mawaziri wanne wamewajibika kisiasa,” alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete aliwapa pole mawaziri hao na kuwapongeza kwa uamuzi wa kukubali kuwajibika kwa makosa yaliyofanywa na maofisa wa chini yao, “Wameonyesha ukomavu wa kisiasa na moyo wa uzalendo.”

Dawa za kulevya

Akizungumzia dawa za kulevya, Rais Kikwete alisema kati Januari na Desemba 2013, kilo 1,261 za heroin, kilo tatu za cocaine na kilo 89,293 za bangi zilikamatwa na watuhumiwa 1,631 kutiwa mbaroni.

“Tupo hatua nzuri katika matayarisho ya kuanzisha Kikosi Maalumu cha Kupambana na Dawa za Kulevya katika mwaka wa fedha 2014/15. Pia tutaitazama upya sheria ya adhabu kwa makosa ya kufanya biashara ya dawa za kulevya ili kuifanya iwe na meno makali zaidi,” alisema.

Akizungumzia usalama wa nchi alisema mwaka 2013 umemalizika bila kuwa na matukio yoyote mabaya na kwamba hata uhusiano wa Tanzania na nchi jirani unaendekea kuwa mzuri.

Pia aligusia suala la ujambazi na kueleza kuwa mwaka 2013 matukio ya ujambazi yalipungua ikilinganishwa na mwaka 2012… “Takwimu zinathibitisha ukweli huo, mwaka 2012 matukio ya ujambazi yaliyoripotiwa yalikuwa 6,872 na kwa mwaka 2013 yameripotiwa matukio 6,409.”

Katiba

Kuhusu Katiba, Rais Kikwete alisema uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba utakuwa umekamilia mwishoni mwa mwezi huu na kwamba baada ya hapo Bunge hilo litaanza.

“Iwapo Rasimu ya pili ya Katiba itakubaliwa na wananchi, hapo tutakuwa tumepata Katiba Mpya. Lakini, iwapo Rasimu itakataliwa ina maana kuwa Katiba ya sasa itaendelea kutumika mpaka hapo mchakato mwingine utakapoanzishwa na Katiba Mpya kupatikana,” alisema.

Akizungumzia Pato la Taifa, alisema limekua kwa asilimia 7.1 ukilinganisha na asilimia 6.9 mwaka jana.

Pato la Taifa

“Tunategemea kuwa mwaka 2014 Pato la Taifa litakua kwa asilimia 7.3. Mfumuko wa bei umeshuka kutoka asilimia 12.1, Desemba, 2012 hadi asilimia 6.2, Novemba 2013. Lengo letu ni kufikia asilimia 5 mwezi Juni, 2014” alisema.

Alisema hadi Novemba, 2013, Tanzania ilikuwa imeuza nje bidhaa na huduma zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 7,720.8 ukilinganisha na Dola milioni 7,916.6 za mwaka ulioishia Novemba 30, 2012.

CHANZO: MWANANCHI