Michezo

Mwakilishi wa Bububu aahidi vifaa kwa timu ya TASWA Zanzibar,

Mwakilshi wa jimbo la Bububu Mh, Hussein Ibrahim Makungu ameahidi kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya chama cha Waandishi wa habari za michezo Zanzibar.

Ahadi hiyo ameitoa leo wakati alipotembelea na kuzungumza na wachezaji pamoja na viongozi wachama hicho katika viwanja vya Maosidung mjini Zanzibar.

Vifaa alivyoahidi kusaidia katika timu hiyo ni pamoja na jezi, soksi pamoja na mipira ili waweze kundelea na mchezo huo kwa lengo la kushajiisha michezo hapa nchini.

Pia amewataka wnamichezo hao kudumu katika mazoezi mbalimbali ili kuweza kujenga afya zao.

Akizungumza katika hafla hiyo msemaji wa timu hiyo Nd, Ramadhan Madogo amesema timu hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa vifaa vya michezo kama mipira, jezi, viatu pamoja na madawa kwa ajili ya mchezaji atakapoumia.

Aidha Nd, Madogo amemtaka Mwakilishi huyo kuwa mlezi wa timu hiyo ili iweze kusonga mbele katika michezo.

Leave a comment